Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba waamua kufanya kweli

SALIM TRY AGAINM.jpeg Salim Abdallah Mhena ‘Try Again’.

Thu, 27 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kabla ya Jumatatu asubuhi Simba yote itakuwa imejulikana. Siku hiyo mapema kabisa itapaa kwenda kambini ‘Pre Season’ nchini Misri.

Hadi sasa imekamilisha usajili wa wachezaji wasiopungua wanne, pia imeendelea kuwapa ‘Thank You’ baadhi ya nyota waliokuwepo kikosini hapo msimu uliopita na kuwaongezea mikataba mastaa wengi.

Arena tunajua Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah Mhena ‘Try Again’, yuko DR Congo  na inaelezwa ameenda kukamilisha dili za wachezaji watatu.

Ni beki wa kati, Idumba Fasika aliyewahi kukipiga Valerenga ya Norway. Mwingine ni Winga Elie Mpanzu kutoka AS Vita.

Unavyosoma hapa, Kigogo na mafia wa usajili wa Simba Cresentius Magori yuko Zambia na tayari amemshusha winga matata Joshua Mutale (22) kutoka Power Dynamos, lakini pia kiungo, Debora Fernandes Mavumbo kutoka Mutondo Stars ya Zambia wote wakisubiri kipyenga cha kuanza kwa kambi ya kujiandaa mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live