Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba vs Yanga; Ni kupambana sio kucheza mpira

ALLY MAYAY TEMBELEE Ally Mayay

Sat, 4 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaimu Mkurugenzi wa michezo nchini ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Yanga Ally Mayay Tembele amesema wanapokutana watani wa jadi nchini huwa ni 50 kwa 50 huku akisema mchezo wao kuwa ni kupamba na sio kucheza mpira

Akizungumza na waandishi wa habari katika fainali za Dkt. Chaya Jimbo Cup zilizofanyika tarafa ya Kintinku wilayani Manyoni mkoani Singida alipomwakilisha Waziri wa Utamaduni sanaa na Michezo Dkt. Damasi Ndumbaro, Mayay amesema utamaduni wa timu hizo zinapokutana ni kupambana zaidi ya kucheza mpira

"Mechi za Simba na Yanga siku zote huwa ni hamsini kwa hamsini siku zote kwasababu ilishathibitika sio mara moja sio mara mbili hata kuna wakati performance labda wewe timu hii hapa labda Yanga inaperform vizuri kweye mechi zingine Simba ipo chini.

"Lakini inapokuja Simba na Yanga unashangaa hii ambayo imeperform vizuri haijapata matokeo chanya au Kuna wakati labda Simba inaperform vizuri Yanga haijafanya vizuri.

"Kwa hizi timu watani wa jadi huwa sio kwenda kucheza mpira ni utamaduni wa kwenda kupambana kucheza mpira unajua kuna kucheza mpira na kupambana kucheza mpira," amesisitaza nguli huyo wa soka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live