Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba vs Ihefu wabadilishwa Muda, sasa kupigwa usiku

Ihefu Waifata Simba Kikosi cha Ihefu

Fri, 7 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baina ya wenyeji, Simba na Ihefu umesogezwa kutoka Saa 10:00 jioni hadi Saa1:00 usiku.

Ikumbukwe mchezo huo ulikuwa upigwe Uhuru lakini umehamishiwa kutoka Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam hadi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam.

Inafahamika Robo Fainali ya mwisho ya michuano hiyo baina ya mabingwa watetezi, Yanga SC na Geita Gold itafanyika hapo hapo Azam Complex Jumamosi Saa 1:00 usiku.

Wakishinda; Simba atacheza na Azam FC aliyemtoa Mtibwa Sugar na Yanga atakutana na Singida Big Stars aliyemtoa Mbeya City.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live