Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba vs Azam, namba hazidanganyi

Fei Toto Fred  Pic Simba vs Azam, namba hazidanganyi

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mara nyingi Azam na Simba zinapokutana imekuwa mechi ambayo ni nadra kumalizika bila nyavu kutikisika.

Kwenye mechi 11 zilizopita za ligi baina ya timu hizi mhezo mmoja pekee uliomalizika bila bao (0-0), mechi nyingine 10 zimemalizika kwa nyavu kutikiswa yakiwa yamefungwa jumla ya mabao 26, Simba ikifunga mengi zaidi (15) na Azam ikifunga 11, huku mchezo uliozalisha mabao mengi ukiwa ule wa Machi 4, 2020 ambapo Simba ilishinda 3-2.

Katika mechi hizo 11 za ligi zilizopita, matokeo ya sare yalitawala lakini hata hivyo Simba iliongoza kwa kushinda ikiibuka na ushindi mara nne huku Azam ikishinda mechi moja tu na sita zilizosalia kumalizika kwa sare.

Azam ndiyo ina matokeo mazuri zaidi katika mechi zake tano za ligi zilizopita kwani imeshinda nne na kutoa sare moja huku Simba ikiwa imeshinda mbili, sare mbili na kupoteza moja katika mechi zake tano za ligi zilizopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live