Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba vs APR ni mtego huo

Simba Squad.jpeg Simba vs APR ni mtego huo

Fri, 5 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi, Simba inashuka dimbani leo kuikabili APR ya Rwanda katika mchezo wa kukamilisha hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Mchezo huo wa kundi B kwenye uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar utafuatia mchezo wa awali kati ya Jamhuri na Jamus.

Simba inaongoza kundi hilo ikiwa na poiti sita baada ya michezo miwili ikifuatiwa na Singida Fountain Gate yenye pointi sita michezo mitatu, APR ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu baada ya michezo miwili wakati JKU ni mwisho haina pointi baada ya michezo mitatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live