Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba vitani kwenda makundi

Bc8f600937bdcdbe2ac281c831f93910 Simba vitani kwenda makundi

Wed, 23 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba itacheza na FC Platinum kwenye uwanja wa michezo wa Taifa, Harare, Zimbabwe leo.

Mchezo huo ambao utaanza majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki ni muhimu Simba kushinda ili kutengeneza mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya makundi.

Safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho leo itaongozwa na Meddie Kagere huku John Bocco akikosekana kutokana na kuwa majeruhi lakini kukosekana kwake hakuwezi kuondoa matumaini ya ushindi kwani kuna wachezaji wengine hatari kama Chris Mugalu.

Simba inajivunia kufika nane bora mwaka juzi baada ya kufanya vizuri katika michezo ya awali.

Ni rekodi inayohitaji kuvunjwa msimu huu baada ya msimu uliopita kushindwa kufanya hivyo na kutolewa hatua za awali.

Akizungumzia mchezo huo jana, Kocha Simba, Sven Vandenbroeck alisema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanashinda lakini watawakosa Bocco na Aishi Manula katika mchezo huo.

"Tuna saa chache kabla ya mchezo, tumejaribu kila njia ili waweze kucheze mchezo huo lakini imeshindana. Bocco bado yupo kitandani hayupo sawa, Aishi aliumia mchezo uliopita na anaweza kuchukua wiki au zaidi kupona," alisema Sven.

Mchezaji mwandamizi wa kikosi hicho, Erasto Nyoni alisema mchezo wa leo watakuwa makini kwa sababu FC Platinum ni timu nzuri. “Naamini kocha amewafuatilia vizuri na sisi kama wachezaji tumejiandaa kukabiliana nao. Kwa uwezo wake Mungu naamini tutafanya vizuri," alisema.

Baada ya mchezo huo Simba itarejea nyumbani kujiandaa na mchezo wa marudiano uliopangwa kuchezwa kati ya Januari 5 au 6 mwakani.

Endapo Simba itaitoa timu hiyo itafuzu robo fainali lakini ikiondolewa itaangukia Kombe la Shirikisho Afrika.

Klabu ya Zamalek ya Misri imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya makundi ya Michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya klabu Gazelle FC ya Chad kujiondoa baada ya serikali ya nchi hiyo kuizuia kusafiri kwenda Misri kucheza na mabingwa hao wa Misri.

Chanzo: habarileo.co.tz