Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba vitani Congo DR leo

A41f404fd185245315d061026490cc09 Simba vitani Congo DR leo

Fri, 12 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Simba leo wanakianza kibarua cha kupigania pointi tatu dhidi ya AS Vita ya Congo DR kwenye mchezo wa kwanza hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Mchezo huo wa kundi A utachezwa saa 4:00 usiku kwenye uwanja wa taifa wa nchi hiyo wa Martyrs of Pentecost uliokuwa unajulikana zamani kama Kamanyola uliopo Kinshasa.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa mwaka juzi hatua kama hiyo ambapo Simba wakiwa ugenini walikula kichapo cha mabao 5-0 na kisha mechi ya marudiano nyumbani kwenye uwanja wa Mkapa wakashinda mabao 2-1.

Ulikuwa ni mchezo wa mwisho wa kuamua nani asonge mbele kwa pointi na ndipo Simba ikasonga.

Leo zinakutana tena zikiwa na tofauti kidogo kuanzia wachezaji, benchi la ufundi kwa hiyo wote watakuwa wameboresha vikosi vyao lakini wakiwa katika viwango tofauti.

Kuna wachezaji kama Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko na wengine hawapo tena katika kikosi cha Vita wakiwa wamewauza na kununua wengine ila kocha wao ni yule yule Florent Ibenge.

Na kwa Simba kuna wachezaji kama Emmanuel Okwi hayupo kikosini ila asilimia kubwa wapo isipokuwa Kocha Didier Gomez ambaye ni mpya ni baadhi ya wachezaji waliosajiliwa.

Simba ambao ni mabingwa mara tatu wa Ligi Kuu Bara bado wapo katika kiwango kizuri baada ya kuonesha ubora katika michezo iliyopita hatua za awali ikiwatoa FC Platnum kwa mabao 4-1. Mchezo wa kwanza walifungwa 1-0 ugenini kisha wakashinda 4-0 nyumbani.

Mchezo mwingine waliiwatoa Plateau United ya Nigeria na kutinga hatua hiyo kwa jumla ya bao 1-0 baada ya mchezo wa kwanza kushinda ugenini 1-0 na kupata suluhu nyumbani.

Timu hiyo inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kwa pointi 39 katika michezo 17 iliyocheza. Michezo yake ya mwisho ya ligi ilishinda dhidi ya Dodoma jiji mabao 2-1 na kupata sare dhidi ya Azam FC ya mabao 2-2.

Wekundu hao wa Msimbazi wapo vizuri zaidi kwenye safu ya ushambuliaji ikiongoza kwenye ligi kwa kufunga mabao 41 mengi kuliko timu nyengine na mshambuliaji wake hatari zaidi ni Medie Kagere anayeongoza kwa kufunga mabao tisa, Cletus Chama akiwa na pasi za mabao tisa na mabao sita, akifuatiwa na Luis Miquissone pasi nane na mabao mawili.

Kwa upande wa Vita iliyocheza raundi moja ilimtoa Young Buffaloes ya Mbabane kwa jumla ya mabao 6-3, mchezo wa kwanza wakitoka sare ugenini mabao 2-2 na kushinda mabao 4-1 nyumbani.

Katika ligi ya kwao inashika nafasi ya tatu kwa pointi 32 katika michezo 14 ikiwa haijapoteza mchezo wowote zaidi ya ushindi na sare.

Yeyote kati ya timu hizo mbili ana nafasi ya kuibuka na ushindi kutegemea na mbinu za kila mmoja dhidi ya mwenzake kwani wote wanastahili kutokana na ubora wao.

Chanzo: habarileo.co.tz