Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba vinara wa kukosa penalti

Bocco Jr John Bocco

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba ,imeingia katika takwimu ngumu wakiwa ndio timu inayoongoza kwa kukosa penalti.

Mpaka sasa Simba imekosa jumla ya penalti 5 huku tatu kati ya hizo wakikosa washambuliaji wao watatu.

Nahodha wa Simba John Bocco pamoja na wenzake Meddie Kagere, Chris Mugalu wameungana na kiungo Rally Bwalya huku beki Erasto Nyoni naye akiwemo.

Biashara wako nyuma ya Simba wao wakikosa penalti mbili kupitia wachezaji wao wawili tofauti Collins Opare na Baron Oketch.

Wachezaji waliokosa penalti mpaka sasa ni pamoja na Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Oketch (Biashara United), Habib Kyombo (Mbeya Kwanza), Boban Zirintusa (Mtibwa Sugar).

Wengine ni Opare (Biashara United), Emmanuel Mvuyekule(KMC), Eliud Ambokile (Mbeya City), Raymond Masota (Geita Gold), Renatus Kisase (Ruvu Shooting), Kagere, Bocco, Bwalya, Mugalu na Nyoni (wote wa Simba).

Chanzo: www.mwananchi.co.tz