Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba sasa wajifunze kucheza ni 'timu ndogo'

Simba Iliboronga Baada Kibu Denis Kuumia   Mkazuzu Simba sasa wajifunze kucheza ni 'timu ndogo'

Sun, 19 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wahenga wanasema ogopa sana kupigana na mtu ambaye anajua wewe ni bora halafu akapata nafasi ya kukupiga, atakupiga kama ngoma.

Mtu anaejua wewe una nguvu ukipigana naye, ukijichanganya anaweza kukuua bila huruma kwa sababu anataka apate heshima lakini pia kuuondoa utawala wako na ukubwa wako kwenye himaya husika.

Simba SC ni timu ya kudharau mambo, waliwahi kushamfunga mtani wao Yanga goli sita, msimu uliopita kwenye hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika, walimfunga Horoya goli saba (7).

Lakini matokeo yale yaliishia pale pale uwanjani kwa Mkapa. Msimu wa mwaka juzi Simba walikuwa hizi goli tano ni kawaida sana kushinda.

Coast Union alikwenda vibaya, akapigwa goli nane (8), lakini bado lilikuwa jambo la kawaida sanaa kwao.

Juzi tu wametwaa Ngao ya Jamii mbele ya mtani wao sijui hata kama mashabiki walifika Airport kupokea ngao.

Wenzao leo wamewakanda goli tano (5-1), ndio mtaji wao wa kuikuza timu yao na Yanga, kupiga pesa kupitia wadhamini kwa kununua haki ya mabango na kutengeneza online contents, Wananchi wana haki ya kujivunia hilo.

Kwa mujibu wa CAF, Yanga wapo ipo chini ya 20 kwa ubora barani Afrika kumfunga timu namba (8) Afrika lazima watambe.

Mamelodi Sundowns ilimfunga goli tano Al Ahly ila kwa sababu Mamelodi ni timu kubwa nalo liliishia pale pale uwanjani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live