Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba ni rekodi na maokoto tu

Simba Sports Clubb Simba ni rekodi na maokoto tu

Sun, 1 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha Simba kinashuka uwanjani leo ikiwa na kazi mbili tofauti kwenye mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

Kwanza ni kupata matokeo yatakayoivusha kuingia makundi na huilo likikamilika litatimiza kazi nyingine ya kuweka rekodi kwa timu za Tanzania katika ushiriki wa michuano hiyo ya Afrika, lakini ikijitengenezea mazingira ya kuvuta mkwanja wa maana kutoka kwa wadhamini.

Baada ya sare ya mabao 2-2 ugenini dhidi ya Power Dynamos, Simba leo ina kibarua cha wastani cha kuwatupa nje Wazambia hao, pale timu hizo zitakaporudiana katika Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni.

Sare tasa na ile ya 1-1 ama ushindi wa aina yoyote ni matokeo yatakayoifanya Simba itinge makundi, hivyo kuboresha rekodi ya kuwa timu ya Tanzania iliyotinga mara nyingi zaidi hatua hiyokwani itakuwa ni mara ya sita, lakini itajihakikisha kuvuna Dola za Kimarekani 700,000 (zaidi ya Sh 1.8 bilioni)

Fedha hizo hupewa timu zilizotinga hatua hiyo baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilipoboresha kuiwango cha fedha za washindi wa michuano ya Ligi ya Mabingwa na ile ya Kombe la Shirikisho amalo kwa Tanzania, Singida Big Stars ndio pekee iliyosalia na ikicheza Saa 12 ikiwa ugenini Misri na kama itashinda itatinga makundi na kujihakikisha Dola 400,000 (karibu Sh 1 Bilioni).

Mechi hiyo kwa Simba ni muhimu na inapaswa kucheza kwa hesabu na tahadhari kubwa hasa katika eneo la ulinzi, pia inatakiwa kuongeza umakini wa kutumia nafasi itakazozitengeneza ili ipate matokeo yatakayoivusha.

Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’, anaingia katika mechi hii akiwa na wigo mpana wa uteuzi wa kikosi cha timu hiyo, kwani atawakosa wachezaji watatu tu kutokana na majeraha ambao ni Aishi Manula, Henock Inonga na Aubin Kramo, lakini bado ana wachezaji wengi wa kumpa matokeo mazuri leo.

Simba inaonekana kuipa uzito mkubwa mechi hiyo hasa ikikumbuka historia mbaya ya kutolewa nyumbani na Jwaneng Galaxy na UD Songo licha ya kushinda na kutoa sare ugenini dhidi yao katika mechi za mwanzo.

Robertinho alisema Simba itapambana kuhakikisha inawapa furaha mashabiki wao.

“Tumepata muda wa kujiandaa na wachezaji wapo katika hali nzuri kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi yatakayotuvusha,” alisema Robertinho.

Kikosi kinachotarajiwa kuanza;

Ayoub Ladred, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein, Kennedy Juma, Che Malone, Sadio Kanoute/Fabrice Ngoma, Kibu Denis, Mzamiru Yasin, Jean Baleke, Clatous Chama na Saido Ntibazonkiza.

Chanzo: Mwanaspoti