Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba ndiyo sababu ya Yanga kushindwa kuujaza Mkapa Stadium - Dauda

Mashabiki Yanga Mil 130 Simba ndiyo sababu ya Yanga kushindwa kuujaza Mkapa Stadium - Dauda

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi nguli wa masuala ya soka nchini, Shaffih Dauda amesema kuwa SC ndiyo chanzo cha Yanga SC kushindwa kuujaza Uwanja wa Mkapa katika Tamasha lao Siku ya Mwananchi.

Tamasha hilo lilifanyika Jumamosi iliyopita ambapo Yanga walitangaza wachezaji wao watakaokuwa nao kuelekea msimu mpya huku wakicheza mechi ya kirafiki na kaizer Chiefs ya Afrika Kuzini ambapo yanga walishinda kwa bao 1-0.

Akizungumzia hilo, Digala amesema; “Simba na Yanga ni wapinzani wa Jadi lakini upinzani kuna sehemu una mipaka sio kwenye kila kitu na huo ushindani ni uwanjani lakini sasa hivi, kuna ushindani mwingine wanahitaji kukaa mezani ishu ya biashara haihitaji ushindani na kutengenezeana shoti.

“Wakati Yanga wanafanya promo ya Tamasha lao Simba wakawa wanatangaza Kibegi ile ikatrend na siku ya tamasha Simba wakazindua jezi watu wakakesha na jezi hiyo kwangu mimi ndio ilikuwa mbinu bora. Wanajiweka sawa kukuonyesha njia ya mafanikio kimpira," amesema Shaffih Dauda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: