Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba ndio wataalamu wa kufuzu Robo Fainali- Ahmed Ally

Simba Ndio Wataalamu Wa Kufuzu Robo Fainali  Ahmed Ally.jpeg Simba ndio wataalamu wa kufuzu Robo Fainali- Ahmed Ally

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa simba SC,Ahmed Ally amesema, Simba ndio klabu yenye utaalamu wa kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika.

Amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi Jumamosi hii pale Uwanja wa Benjamini Mkapa kwa ajili ya kuishangilia timu yao itakapokuwa inavaana na Jwaneng Galaxy mchezo wa kuamua hatma ya Simba kufuzu Robo Fainali ya Klabu Bingwa.

“Sisi ndio wataalamu wa namna ya kufuzu robo fainali. Tumekuja hapa kuwambia umuhimu wa Wanasimba wote kujitokeza kwa wingi Jumamosi ili tukaandike historia ya kufuzu robo fainali mara tano mfululizo tukiwa pamoja," alisema Ahmed Ally akiongea na Wanasimba wa Mbezi Luis.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live