Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba ndio basi tena, yabanwa mbavu na Polisi TZ

Simba FT Moshi Mchezo umemalizika kwa sare ya bila kufungana

Sun, 10 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pengine unaweza kusema sare ya leo imeweka mazingira magumu kwa Simba SC kutetea ubingwa wake msimu 2021/2022.

Tofauti ya alama baina ya Simba na Kinara wa Ligi Kuu kwa sasa ni alama 10, baada ya kila timu kushuka di,mbani michezo 19, huku Simba akijikusanyia alama 41 na Yanga akiwa kileleni na alama 51.

Simba imetoka sare ya bila kufungana na Polisi Tanzania katika Uwanja wa Ushirika mjini Moshi jioni ya leo.

Mwalimu Pablo Franko amelalamikia Uwanja pamoja na ratiba kwa upande wao huku akisisitiza kuwa mipango yao ni mechi ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho dhidi ya Orlando Pirates April 17.

Pengine Polisi wangeweza kuondoka na alama tatu kama nafasi waliyoipata dakika za lala salama wangeweza kuitumia vyema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live