Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba ndio Mabingwa wa kimbe waliloliandaa (+picha)

Simbasctanzania 143825384 899543217541350 6013735732624581334 N 660x400 Simba ndio Mabingwa wa kimbe waliloliandaa (+picha)

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Klabu ya soka ya Simba SC imeibuka Mabingwa wa michuano ya Simba Super Cup baada ya kufikisha pointi 4 ambazo hazijafikiwa na washiriki wengine Al Hilal na TP Mazembe.

Mashindano hayo yamehitimishwa leo Januari 31, 2021 kwa mchezo kati ya Simba SC dhidi ya TP Mazembe ambao umemalizika kwa suluhu na Simba SC kuibuka mabingwa.

Mfungaji bora wa michuano amekuwa Bernard Morrison akifunga magoli mawili, huku mchezaji bora wa mashindano akiwa ni Rally Bwallya.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Simba SC Barbara Gonzalez, amesema kuwa kwa kiasi kikubwa malengo ya michuano hiyo yametimia ambayo ilikuwa ni kujenga utimamu kwa wachezaji kuelekea hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba ipo kundi A na timu za As Vita ya DR Congo, Al Ahly ya Misri na Al Merrick ya Sudan.

Chanzo: millardayo.com