Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba ndani ya Morocco kujiandaa na Msimu Mpya

Wachezaji Wa Simba Wachezaji wa Simba Sc

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Soka ya Simba inajiandaa kusafiri kuelekea Nchini morocco kuweka kambi kwa siku kumi (10) ikijiandaa na msimu mpya wa 2021/2022.

akizungumza na kipindi cha michezo cha Sports Headquarter,Kinachorushwa na Kituo cha Redio cha E-fm,Mwenyekiti wa Klabu hiyo Murtaza Ally Mangungu amesema wachezaji wote wa simba wameshawasili kutoka katika mapumziko na wameanza kutekeleza ratiba iliyopangwa na benchi la ufundi na viongozi kwa ujumla.

Mangungu amesema Timu itaondoka kuelekea morocco kwa ajili ya kuweka kambi kwa muda wa siku kumi (10) na tayari Mtendaji mkuu wa Timu hiyo mwanamama Babra Gonzalez, yupo nchini Morocco kwa siku kadhaa sasa akifanya maandalizi kwa ajili ya timu hiyo.

"Tunakwenda Morocco kwa ajili ya facility (Miundombinu),utulivu na pia relaxation ya eneo hilo,taarifa ya lini timu itaondoka itatoka hivi karibuni ndani ya wiki hii pengine ni kwa sababu mimi niko nje ya timu kwa sasa kutokana na majukumu mengine ndio maana bado sijajua itatoka lini lakini mtafahamishwa" amesema Mangungu.

Simba ambao ndio mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Tanzania Bara,watashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika hivyo maandalizi kama hayo ni nafasi nzuri kwao kujifunza namna nchi zilizoendelea kisoka zinavyojiandaa na kuendesha klabu zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live