Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba na saa 48 za maangamizi

Simba Kimkakati Simba na saa 48 za maangamizi

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba Mbrazili, Roberto Oliveira 'Robertinho' amewachimba mkwara mastaa wa kikosi chake na kuwaambia hataingia kwa mazoea kwenye mechi dhidi ya Yanga Jumapili ijayo wala kuangalia matokeo ya mechi zilizopita.

Anasema hata kama staa alikuwa anafanya vizuri siku za nyuma, lazima aonyesha kiwango bora katika mazoezi ya siku tatu kuanzia jana ndio atapata nafasi ya kucheza mechi hiyo.

Mwanaspoti linajua, Robertinho aliwaweka kikao wachezaji baada ya mechi na Ihefu iliyomalizika kwa Simba kushinda 2-0, kwa mabao ya Jean Baleke na kuwataka kujituma zaidi akiamini mechi na Yanga ni ya heshima na zawadi kwa mashabiki wa Simba hivyo hataki mzaha wala mazoea kabisa.

Katika kikao hicho, Robertinho aliwataka wachezaji wote kuuchukulia mchezo huo kama fainali kwao na ambaye atakuwa na masihara mazoezini basi asitegemee kupata namba katika mechi hiyo na wala kigezo cha kucheza vizuri mechi zilizopita si kigezo.

"Najua kila mmoja anaitaka mechi hii, ni mechi ya sifa kwenu na faida kubwa lakini niwahakikishie ambaye hatakuwa makini anaweza aishie jukwaani na nitawashangaza," aliwaeleza wachezaji.

Robertinho ameliambia Mwanaspoti kuwa kusimamia nidhamu na uwajibikaji wa wachezaji katika mazoezi ndiyo msingi ambao huakisi namna mechi itakavyokuwa.

"Ujue mimi nina uzoefu wa kutosha na mechi za namna hii na nimenyooka, Simba inawachezaji wengi walio bora lakini wapo pia ambao bado hawajitumi kwa kiasi ninachokitaka.

Siku zote nawaambia wachezaji wangu, tusiishi kwa mazoea na hivi ndivyo ilivyo, ambaye hatafanya vizuri mazoezini sitampa nafasi kwenye mechi ijayo na wote wanajua hilo na hadi sasa kila mmoja yupo tayari kupambana hadi mwisho," alisema Robertinho na kuongeza;

"Tunafanya maandalizi ya siku tatu lakini mechi inachezwa kwa dakika 90 tu, hivyo ni jambo gumu lakini jepesi kwa namna nyingine, sio tu kuwashangaza wachezaji kwa namna nilivyokuwa mkali, naweza pia nikawashangaza wadau wa soka baada ya dakika 90 za mechi hiyo kwani tunaichukulia kwa uzito mkubwa na naamini tutashinda."

Simba na Yanga zitakutana katika mechi hiyo ikiwa ni ya pili kukutana kwenye ligi msimu huu ambapo Yanga ipo kileleni mwa msimamo na alama 68 huku Simba ikikaa nafasi ya pili na pointi 60 na katika mechi ya mzunguko wa kwanza zilipokutana zilitoshana nguvu kwa kufungana 1-1 kwa mabao ya Agustine Okrah (Simba) na Stephane Aziz Ki (Yanga).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live