Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba na hesabu zao ziko hivi

Simba Sports Club Bunju Arena.jpeg Simba; Hesabu zao ziko hivi

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kufanya vizuri kwenye mechi zote ambazo watacheza.

Kwa sasa Simba inashiriki Kombe la Mapinduzi ambapo imetinga hatua ya robo fainali ikivunja rekodi yake mbovu ya kukwama kufika katika hatua hiyo 2023.

Ni mchezo dhidi ya Jamhuri itakuwa katika hatua ya robo fainali ambapo unatarajiwa kuchezwa Januri 8 2024 ikiwa watapata ushindi watakata tiketi kutinga hatua ya nusu fainali.

Ally amesema:”Wachezaji wanatambua kazi iliyopo ni kutafuta ushindi na tunaamini itakuwa hivyo mpaka tutakapokamilisha malengo, ushindani ni mkubwa nasi tunaendelea kufanya maandalizi mazuri,”.

Miongoni mwa wachezaji waliopo na kikosi cha Simba kwenye Mapinduzi 2024 ni nahodha John Bocco, Shomari Kapombe, Ally Salim, Moses Phiri, Sadio Kanoute.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live