Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba mwambieni Mo Dewji awaachie timu yenu - Luambano

Mo Dewji Uwanjani 1140x640 Mo Dewji

Wed, 10 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa michezo wa kituo cha radio cha Clouds FM, Alex Luambano amesema kuwa tatizo lililopo Simba SC kwa sasa ni mwekezaji wao Mohammed Dewji 'Mo' kwani ameshindwa kutoa pesa kwa ajili ya usajili na uendeshaji wa mambo mbalimbali ya timu na na kuitelekeza timu kwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo.

Luambano amesema hiyo ndiyo sababu kubwa ya Simba SC kuyymba na kupata matokeo mabovu ikiwemo kuishia robo fainali ya CAFCL, na robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank.

"Kama mashabiki wa Simba wanataka suluhu, aambiwe Mo aiache timu au arudi afanye kazi kwenye nafasi yake na kwa mfumo uliopo wanaweza wakarudi kubadilisha mfumo wa uwekezaji.

"Uwekezaji wa mtu mmoja kushika share zote (49%) unamtengenezea nguvu yakuona yeye ndio ana-power.

"Yanga waliliona hilo na kwenye uwekezaji wametoa nafasi kwenye zile 49% kwa mtu zaidi ya mmoja, ukimuweka mmoja anajiona yeye ndio mmiliki na hiki ndicho kinachowakuta Simba.

"Mo anaweza kutaamka timu nimeinunua, Wanasimba nawaambia leo, muyafute Mo mumwambie awaachie Simba yenu au arudi kwenye nafasi yake.

"Na kingine mrudi muangalie kwenye mfumo wenu wa uwekezaji mbadilishe mfumo uruhusu wengine kuingia," amesema Luambano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live