Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba msimvunjie heshima Benchikha kisa Mgunda

Benchikha Msz Simba msimvunjie heshima Benchikha kisa Mgunda

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ushauri wangu kwa wanasimba, baada ya matokeo ya mechi za karibuni kuwa mazuri wengi wanamsema sana kocha Benchikha na kumshushia lawama sana, nadhani kama mashabiki mnapaswa kumpa heshima yake Benchikha tusimvunjie heshima na kuona Mgunda kama yupo vizuri kuliko yeye kwasababu ya matokeo ya mechi hizo chache.

Wakati mwingine mnawaamimisha viongozi baadhi ya vitu alafu ninyi wenyewe baadae mnawataka tena wajiuzulu, unamshangaa shabiki anasema Benchikha alikuwa anaua vipaji vya wachezaji je mnadhani Mgunda akiachiwa hii timu na hawa wachezaji anaweza kuwafunga Yanga? Al Ahly nk? Nafikiri badala ya kumponda Benchikha tutumie muda mwingi kushauri usajili bora na uboreshwaji wa benchi hilo la ufundi.

Kutengeneza profile kama alivyofanya Benchikha kwenye football field siyo jambo dogo kwahiyo haitakiwi kumzungumza kila wakati as if Sasa Simba inacheza kama man city na pia tusimuone kama alikuwa kocha mdogo badala yake tudeal na matatizo yaliyokuepo kwanza.

Mkiendelea kujiaminisha kuwa kila kitu kimetulia baada ya Benchikha kuondoka mtarudi tena kutukana mbeleni hapo na viongozi wanapenda kusikiliza Zaidi mnachokitaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live