Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba msije na nia ya kuwapiga viongozi wenu - Kamwe

Kamwe Msc Simba msije na nia ya kuwapiga viongozi wenu - Kamwe

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amewasihi mashabiki wa Simba kutoenda uwanjani na mawazo ya kuwapiga/kuwashambulia viongozi wao iwapo watafungwa kwenye mchezo wao wa dabi, Jumamosi Aprili 20.

Kamwe amesema hayo baada ya baadhi ya mashabiki kudai kuwa iwapo watafungwa na watani zao Yanga katika mchezo huo, basi watawashushia kipigo viongozi wao wa Simba humo humo kwenye Dimba la Benjamin Mkapa.

Simba kwa sasa wanapitia wakati mgumu baada ya kucheza mechi nne mfululizo bila kushinda huku wakitolewa kwenye michuano ya CAFCl na Kombe la Shirikisho Tanzania.

"Ni tabia ya kishamba mpira umeisha mnawapiga viongozi, achaneni nayo njooni tuangalie mpira. Tuliwapiga tano mkaondoka vizuri tu majumbani kwenu njooni mungalie mpira.

"Tukishinda sisi tutawatania mkitufunga tutaondoka nyumbani, lakini msije na 'mentality' kwamba Yanga wakitufunga humu ndani kunakuwa uwanja wa vita hapana," amesema Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live