Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba mpyaa Mnahesabu hukoo?

Mutale Mq.jpeg Joshua Mutale

Wed, 3 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tayari Joshua Mutale kiraka wa Zambia ameshatambulishwa rasmi Msimbazi. Jana mchana ilikuwa zamu ya Steven Mukwala, staa wa Uganda.

Lakini sasa unaambiwa Simba imetuma tiketi mbili za ndege katika mataifa mawili tofauti ili kuwashusha nchini wachezaji wawili matata akiwemo mrithi wa Clatous Chama aliyetanga-wa kujiunga na Yanga, juzi.

Kati ya tiketi hizo moja imeenda Kinshasa, DR Congo kwa winga Elie Mpanzu ambaye niliripoti dili lake kitambo sana na nyingine imetumwa Abidjan, Ivory Coast kwa kiungo mshambuliaji Jean Charles Ahoua (22), anayetazamiwa kuwa mrithi wa Chama pale Msimbazi.

Msimu uliopita aliibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Ivory Coast tuzo ambayo msimu uliopita ilichukuliwa na Pacome Zouzoua na msimu mmoja nyuma aliibeba Stephen Aziz Ki na wote sasa wanacheza Yanga. Katika msimu huo, Ahoua alifunga mabao 12 na kutoa pasi za mwisho sita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live