Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba mpya inakuja

Mashabiki Wa Simba Kuwa Wageni Rasmi Dhidi Ya ASEC Mimosas Simba mpya inakuja

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba chini ya Mwenyekiti wao Salim Abdallah ‘Try Again’ juzi ilikutana na wanachama waandamizi na kuafikia ajenda mbili za kufanyiwa kazi haraka.

Kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na wanachama 80 kutoka mikoa mbalimbali nchini kama wawakilishi,kilifanyika kwenye ukumbi wa klabu hiyo uliopo mtaa wa Msimbazi, Kariakoo.

Makubaliano ni kwamba mabadiliko ya Katiba yafanyiwe kazi haraka ambapo itaundwa kamati itakayoanza kushughulikia mchakato kwani ina mapungufu ambayo yanakwamisha mchakato wa uwekezaji.

Ajenda nyingine ya kufanyiwa kazi kwa haraka ni kuunda Kamati ya kutatua migogoro na mpasuko ndani ya klabu. Ustadhi Masoud ambaye ni Mwenyekiti wa wanachama hao ameliambia Mwanaspoti kuwa; “Hata tukiwaondoa akina Try Again na Mangungu, bado mpasuko utakuwepo, hivyo tumekubaliana kuyamaliza haya haraka.

“Hizi kamati mbili zitakazoundwa zinategemeana maana huwezi ukaanza mchakato wa marekebisho ya Katiba wakati kuna mpasuko, hivyo lazima haya yafanyike haraka ili tusonge mbele, ila kiufupi tofauti zetu zote tumezimaliza na sasa Simba ni moja,” alisema Masoud.

Alisisitiza kuwa upande wa wanachama leo Jumatano watakutana ili kuchagua wawakilishi wao watakaounga na wale watakaotoka kwenye Bodi kuunda kamati hizo mbili.

Chanzo: Mwanaspoti