Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba mchukueni Pacome

Saido Pacomesss Simba mchukueni Pacome

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wengine watafurahia kuona kasi ya Maxi Nzengeli akiwatesa walinzi, ama Stephen Azizi Ki akipiga ile mipira yake chonganishi ya kuzunguka ambayo inawapa majina ya bahasha makipa.

Wengine wanafurahi kuona krosi tamu za Attohoula Yao zenye mchanganyiko wa maziwa na asali mbichi zikitua kwenye kichwa cha Kennedy Musonda na kwenda nyavuni.

Pacome Zouzoua ni kiungo mshambuliaji ambaye ana vitu vingi ambavyo vinaipa faipa timu yake. Hakai na Mpira ili kupoteza muda yeye huweka mpira sehemu salama kwenye njia sahihi ili timu yake ipate faida.

Uwepo wake ndani ya Dimba una ifanya timu yake ku-control mchezo itavyo Kwa sababu Wana mtu ambaye kazi yake ni kulainisha vitu vyenye kutu.

Navutiwa na ubora wake wa kupiga pasi sahihi zenye macho, uwezo wa kutikisa nyavu na hodari wa kutengeneza mashambulizi.

Pacome akiwa Dimbani huifanya Yanga kuwa na utulivu wa kutosha kwa sababu wanajua mpiga Solo yupo ambaye atawapa furaha mashabiki.

Sitashangaa Klabu ya Simba sc wakibisha hodi na kuhitaji saini ya Pacome kwa uwezo aliokuwa nao dhaili Simba sc anawafaa Pacome Zouzoua na si kuendelea kubaki na mzee wa Bujumbula ambaye kwa sasa soka limekwisha mguuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live