Kikosi cha Simba mara tu baada ya kumalizika kwa mchezo wake dhidi ya Vipers kutoka nchini Uganda, hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo wameibuka na ushindi wa bao 1-0, fasta tu wakavuta mkwanja wao.
Simba wamechukua kiasi cha Tsh Milioni tano za Rais Samia baada ya kufunga bao moja katika mchezo huo wa kundi C.
Mara baada ya kutamatika kwa mtanange huo, Aliekuwa mgeni Rasmi katika mchezo huo Naibu Waziri Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Hamis Mwinjuma alipokea kitita hicho kutoka kwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa na kuzikabidhi kwa Nahodha wa Simba, John Bocco.
Fedha hizo ni ahadi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambae aliahidi kununua kila goli kwa Tsh Milioni tano kwa vilabu vinavyoshiriki Michuano ya Kimataifa.