Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba mambo magumu tena Kaitaba, waambulia sare

Simba Wakishangi.jpeg Simba mambo magumu tena Kaitaba, waambulia sare

Sun, 12 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba SC imeambulia sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Kagera Sugar kwenye muendelezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara

Sare hiyo imewafanya Simba SC kufikisha alama 57 sawa na Azam FC wakisalia kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo nyuma ya Azam FC wenye wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa.

Simba SC watajilaumu wenyewe kwa kukosa nafasi za wazi kwenye mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji wake Fred aliyekosa nafasi 3 za wazi.

Sasa michezo minne imesalia kutamatisha ligi hiyo ambayo kama Azam FC wataitumia vizuri basi watajihakikishia tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live