Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba malalamiko, Yanga maandalizi , Tukutane Disemba 11

Senzo Mbatha Kaimu Mtendaji Mkuu Yanga, Senzo Mazingisa

Wed, 8 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku moja baada ya kuvuja kwa barua iliyoandikwa na uongozi wa Simba SC kwenda kwa TFF/Bodi ya Ligi wakitaka ufafanuzi juu ya Mkataba wa Mdhamini mwenza ambae ni GSM, ili kufanya maamuzi ya kuvaa logo ya mdhamini huyo.

Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mbatha amebainisha kwamba hawana presha na watani zao wa jadi, Simba kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Desemba 11, mwaka huu.

Akizungumza Senzo amesema kuwa wanatambua kuhusu mchezo huo kwa kuwa upo kwenye ratiba, hivyo watafanya maandalizi mazuri ili kupata ushindi.

“Ipo wazi kwa muda mrefu kwamba lazima tutakutana na Simba kwenye mechi ya ligi, hivyo hakuna presha kuelekea mchezo huo, kila kitu kinakwenda sawa na maandalizi yake ni kama ilivyo kwenye michezo mingine.

“Mwendo ambao tunakwenda nao ninaamini kwamba mashabiki wanaona, hivyo hakuna haja ya kuwa na mashaka juu ya uwezo wa wachezaji wetu ambao wapo kwani kila mmoja anafanya kazi kwa umakini katika kutimiza majukumu yake,” alisema Senzo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live