Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kuzoa fedha za Caf

Simba Pic Data Simba kuzoa fedha za Caf

Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thobias SebastianMore by this AuthorBy Charles AbelMore by this Author Dar es Salaam. Siku tatu zimebaki kabla ya Simba kufahamu hatma yake katika Ligi ya mabingwa Afrika kama watasonga katika hatua ya makundi au wataishia hapo, kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya FC Platinum kutokea Zimbabwe ambao mechi ya kwanza walishinda bao 1-0, wakiwa nyumbani kwao.

Shirikisho la soka Afrika (CAF), ambalo linaandaa mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya klabu linaonyesha kuwa timu 16, ambazo zitatinga hatua ya makundi wanajihakikishia kuchukua Dola za kimarekani 550,000, sawa na Sh1.2 bilioni bila kujali kama watafuzu robo fainali.

Simba kama watafanikiwa kutinga hatua ya makundi na wakafanya vizuri na kufika robo fainali kama ilivyokuwa mwaka juzi CAF, watawaongezea fedha hizo na kufika, Dola 600,000 (Sh1.3 bilioni).

Fedha hizo zote ambazo CAF, wanazitoa ni kwa ajili ya maandalizi ya kila timu katika mahitaji yake ya msingi kama nauli ya kutoka eneo moja kwenda lingine, posho kwa wachezaji na benchi la ufundi, kuweka kambi mahala ambapo wanahitaji pamoja na mambo mengine yote ya msingi.

Kama Simba watatinga katika hatua hiyo ya makundi au kusonga mbele itakuwa faida na heshima kwa timu, mchezaji mmoja mmoja na kuweka rekodi nyingine kwa kizazi cha sasa kufika hatua ya makundi kwenye mashindano hayo katika miaka ya karibuni.

Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere alisema pesa hiyo ambayo inatolewa na CAF, inaongeza maroli ya kila timu kushindana kadri ambavyo wanaweza katika mashindano hayo ili kufika mbali ndio maana kuna baadhi ya timu malengo yao ya kwanza ni Ligi ya Mabingwa.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz