Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kuwakosa mastaa wawili mechi ya Vipers

Meneja Simba Ahmed Ally 2 (600 X 628) Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally

Mon, 6 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC, Kibu Denis atakosekana katika mchezo wa marudiano wa mzunguko wa nne hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Vipers FC ya nchin Uganda.

Kibu ambae aliumia katika mchezo dhidi ya Vipers hao hao uliopigwa katika Uwanja wa St.Marys Uganda.

Mbali na Kibu pia Kiungo mkabaji Ismail Sawadogo atakosekana katika mchezo dhidi ya Vipers.

Akizungumza kuelekea mchezo huo Meneja Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally kupitia kipindi cha michezo cha Sports Arena amesema;

"Kuelekea Mechi ya kesho dhidi ya Vipers tutamkosa Mfalme wa Entebbe, Kibu Denis pamoja na Ismail Sawadogo"

Mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Vipers utapigwa kesho Machi 7 katika Uwanja wa Bebjamin Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live