Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kutoka 'Mwakarobo' mpaka 'Kombe la looser'

Simba Msgz Simba kutoka 'Mwakarobo' mpaka 'Kombe la looser'

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kumaliza kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya JKT Tanzania, Wekundu wa Msimbazi Simba SC wameishia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara na hivyo ni rasmi watashiriki michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Licha ya kuuanza msimu vyema wekundu hao walipoteana baada ya kipigo cha 5-1 kutoka kwa mahasimu hao Yanga SC na kujikuta wanamaliza msimu wakifundishwa na makocha wanne tofauti. (Robertinho, Daniel Cadena, Benchikha na Mgunda).

Matajiri wa jiji la Dar es Salaam Azam FC wamefanikiwa kumaliza wa pili kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi muhimu wa 2-0 kwenye mchezo wa mwisho wa ligi hiyo dhidi ya Geita Gold FC

Azam FC wamemaliza na alama 69 na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa Afrika msimu ujao.



Takwimu Azam FC

Mechi - 30

Alama - 69

Mechi walizoshinda -21

Sare - 6

Kupoteza - 3

Mabao ya kufunga - 63

Mabao ya kufungwa - 21

Tofauti ya mabao - 42

Nafasi - 2.

Takwimu Simba SC

Mechi - 30

Alama - 69

Mechi walizoshinda -21

Sare - 6

Kupoteza - 3

Mabao ya kufunga - 59

Mabao ya kufungwa - 25

Tofauti ya mabao - 34

Nafasi - 3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live