Klabu ya Simba SC kutoka Tanzania ni miongoni mwa timu 10 barani Afrika ambazo hazitaanzia raundi ya mtoano (Preliminary Round) kwenye michuano ya CAF Champions League msimu huu na badala yake wataamzia raundi ya pili.
Katika timu hizi 10 kila moja itacheza mechi mbili za Nyumbani na Ugenini kwa mpinzani Mmoja tu, na matokeo ya Jumla yataamua nani atatinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Timu hizo ni
1. Al Ahly SC 2. Wydad AC 3. Esperance 4. Mamelodi Sundowns 5. Simba SC 6. Petro 7. Tp Mazembe 8. Enyimba 9. CR Belouizdad 10. Pyramid FC.
Timu hizi kumi kumi haziwezi kukutana zenyewe katika hatua hiyo ya pili. Lakini kwa upande wa Yanga SC itaanzia hatua ya kwanza (Preliminary round) kwenye michuano hiyo.