Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kutangaza kipa mwingine kabla ya SImba Day

Jefferson Luis Szerban.jpeg Simba kutangaza kipa mwingine kabla ya SImba Day

Thu, 3 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya SImba imesema kuwa itamtangaza kipa mpya kabla ya kufikia siku ya Tamasha la Simba Day litakalofanyika Jumapili ijayo Agosti 6, 2023 katika Dimba la Mkapa.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano Klabu ya Simba, Ahmed Ally ikiwa ni siku chache baada ya kuachana na aliyekuwa kipa wao, Jefferson Luis raia wa Brazil aliyedumu Simba kwa wiki moja tu tangu asajiliwe.

"Suala la golikipa tutatoa taarifa muda sio mrefu, kabla ya Tamasha la Simba Day kila kitu kitakuwa kimewekwa hadharani," amesema Ahmed Ally.

Simba imeachana na golikipa Jefferson Luis aliyebainika kuwa na majeraha ambayo yatamuweka nje kwa muda mrefu.

Luis alisajiliwa hivi karibuni kama mbadala wa kipa namba moja wa Simba. Aishi Salum Manula ambaye yupo nje akijiuguza baada ya kufanyiwa upasuaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live