Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kushusha watatu

Mgunda Pic Siri Kocha wa Simba Juma Mgunda

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Uongozi wa Simba umeanza kufanya maboresho ya Benchi la Ufundi ambapo sasa wamemshusha rasmi kocha wa makipa Zakari Chlouha kutoka Morocco.

Simba haikuwa na kocha wa makipa kwa muda sasa tangu walipoachana na Mohammed Rachid aliyeondoka Septemba 6 mwaka huu na kumchukua Shilton ambaye amekumbana na kasheshe kubwa na mamlaka za dawa za kulevya nchini(soma hapa kushoto).

Siyo huyo tu aliyetambulishwa juzi, Simba inashusha makocha wengine wawili kufikia wikiendi hii ambapo mmoja ni Kocha Mkuu na mwingine ni wa viungo ambao wote hawajuani lakini wana rekodi nzuri kwa mujibu wa viongozi.

Chlouha aliyetambulishwa juzi jioni, alizaliwa Februari 5, 1970 ametokea Al-Urooba ya Falme za Kiarabu huku akihudumu kwenye cheo hicho tangu 2019 akiwahi pia kufanya kazi klabu ya Hassania Agadir ya nchini kwao.

Mojawapo ya mafanikio makubwa akiwa na kikosi hicho ni kuifikisha robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (2018-2019) na nusu fainali (2019-2020)

Habari zaidi zinaeleza kuwa kocha wa viungo atatangazwa kabla hata ya kocha mkuu, ambapo kocha huyo atachukuwa nafasi ya Sbai Karim waliyeachana naye.

Kuhusu Kocha Mkuu taarifa zilizopo ni kwamba naye kila kitu kinakwenda sawa bado tu muda wa kutua nchini kusaidiwa na Juma Mgunda.

Kutokana na Mgunda kuwa kocha msaidizi, Seleman Matola ambaye alikuwa kwenye nafasi hiyo anakwenda kusoma leseni ‘A’ ya CAF huku akipewa ruhusa ya kuendelea nao akimaliza masomo yake au kuamua kutafuta changamoto sehemu nyingine.

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Ahmed Ally ili kuzitolea ufafanuzi juu ya taarifa hizo alisema kila kitu kimekamilika sasa wanashusha chuma kimoja baada ya kingine malengo ni kimataifa na ligi ya ndani.

Chanzo: Mwanaspoti