Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema klabu hiyo ina mpango wa kusajili wachezaji wanne wa Kimataifa wenye viwango vya juu, ili kukiboresha kikosi chao kwa msimu ujao wa 2022/23.
Kiongozi huyo ameanika mpango huo huku Simba SC ikihusishwa na harakati za kuwasajili Wambuliaji Moses Phiri kutoka Zambia na klabu ya Zanaco FC pamoja na Adebayor Zakari Adje ‘Adebayor’ kutoka Niger na klabu ya Union Sportive Gendarmerie Nationale ‘USGN’.
Try Agein amesema miongoni mwa wachezaji waliodhamiria kuwasajili wawili ni Washambuliaji wa Kati, Kiungo Mshambuliaji Mmoja na Beki wa Kati Mmoja.
“Mpango Wetu katika Dirisha Lijalo, tutasajili Wachezaji wanne wa Daraja la Juu wakimataifa Ambao ni mastraika wawili, Winga mmoja na Beki wa kati mmoja. Ni Wachezaji haswa na watakuwa na mchango Mkubwa kwa timu.”
Kwa mantiki hiyo Simba SC itawatema wachezaji wanne wa Kimataifa mwishoni mwa msimu huu, ili kupisha usajili mpya wa Wachezaji watakaoongeza nguvu kwenye kikosi cha Wababe hao wa Msimbazi.