Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kushusha mashine nyingine tatu!

SEMAJI Simba kushusha mashine nyingine tatu!

Thu, 14 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Simba SC, ahmed Ally ametamba kuwa, baada ya kumsajili kiungo mshambuliaji Augustine Okrah kutoka Ghana, wanatarajia kushusha mashine nyingine mpya tatu.

Ahmed amefunguka hayo leo Julai 14, 2022 akiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar wakati kikosi kilipokuwa kikijiandaa kukwea pipa kuelekea nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

“Hatujamaliza bado kuna mashine nyingine tatu zinakuja. Kuna ambao watajiunga na timu kulekule Misri na wengine watatokea hapa,” alisema Ahmed.

Msemaji huyo wa Simba amesema, watakaa nchini Misri kwa takriban wiki tatu kisha watarejea nchini kwa ajili ya wiki ya Simba Day na hatimaye kuanza ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live