Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kuondoka nchini kesho

Ahmed Ally 23 Simba kuondoka nchini kesho

Mon, 10 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, kesho wanatarajia kuondoka nchini kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi.

Hayo yamebainishwa leo Julai 10, 2023 na Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally alipokuwa akieleza mikakati yao kuhusu maandalizi ya msimu ujao.

"Kikosi kitaondoka nchini kesho na wachezaji wote ambao tumewasajili na wale wa zamani. Benchi la ufundi chini ya Roberthinho limeshakamilika, kilichobaki ni safari tu," alisema Ahmed.

Ahmed alisema kikosi kitaa nchini humo kwa takriban wiki tatu kabla ya kurejea nchini Agosti Mosi, 2023 kwa ajili ya tamasha la Simba Day na mechi ya ufunguzi wa Ligi msimu 2023-24 dhidi ya Singida Faountain Gate Agosti 10, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live