Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kuondoka kesho kuifata Singida

81682 Pic+singida Simba kuondoka kesho kuifata Singida

Fri, 25 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIKOSI cha Simba kitaondoka hapa Dar es Salaam, kesho asubuhi kuelekea Arusha ambapo watacheza mechi ya sita Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United ambao wanatumia uwanja wa Sheikhe Amri Abeid kama uwanja wao wa nyumbani. Kikosi hiko kitaondokana na ndege asubuhi wakiwepo wachezaji wote ambao watakwenda kutumika katika mechi ya Singida kabla ya kuanza tena safari nyingine ya kuelekea Shinyaga ambapo huko napo watacheza mchezo mwingine na Mwadui. Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu, alisema kikosi chao kitaondoka kesho Jumamosi na watafika asubihi moja kwa moja watakwenda hotelini na jioni watafanya mazoezi mepesi ya kuweka mwili sawa kwa ajili ya mchezo Jumapili. Rweyemamu alisema wachezaji wataondoka wote ili hata wale wengine ambao walikuwa na majeruhi waweze kupata muda wa kufanya mazoezi na wenzao na kuhusu suala la kutumika au kutokutumika hilo litategemea na maamuzi ya kocha mkuu. "Kuhusu uwanja ambao tunatakiwa kuutumia katika mechi utakuwa na shughuli nyingine hilo lipo nje ya uwezo wetu kubwa ambao lipo kwetu tunafahamu tutautimia uwanja huo kwa ajili ya mechi na kama kutakuwa na mabadiliko watatupatia wenyewe wahusika wa hili," alisema. "Kiujumla maandalizi yote kwa upande wetu yamekwenda sawa na tutafanya mazoezi ya mwisho hapa Dar es Salaam, leo kabla ya kuanza safari ya kwenda Arusha ambapo kiu yetu ni kuona tunaendeleza wimbi na kuvuna pointi tatu," alisema Rweyemamu.

Chanzo: mwananchi.co.tz