Simba mapema tu wamepiga hesabu za kukiboresha kikosi hicho na imebainika ni kuwa wameanza mazungumzo na winga matata wa As Vita, Eric Kabwe kwa ajili ya kuliimarisha eneo lao la ushambuliaji.
Hii sio mara ya kwanza kwa Simba kukamilisha usajili wa mchezaji mapema kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa, kwani wamewahi kufanya hivyo kwa Moses Phiri.
Simba ilikamilisha usajili wa Moses Phiri miezi mitatu kabla ya usajili mkubwa kufunguliwa na sasa imeanza rasmi mazungumzo na uongozi wa mchezaji huyo anayekipiga ndani ya AS Vita ambao wanashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Chanzo chetu kutoka DR Congo kimefunguka kuhusu taarifa za Kabwe kutakiwa na uongozi wa Simba huku wakiweka wazi juu ya Simba kuanza rasmi mazungumzo na uongozi unaomsimamia winga huyo.
“Simba wanamhitaji winga huyu na tayari mazungumzo yameanza rasmi kwa wakilishi wa pande zote mbili za Simba na mchezaji kukutana na kuzungumza jinsi ya kukamilisha usajili wa mchezaji huyo.
“Kabwe ni moja kati ya mastaa wa sasa wa AS Vita, ni moja kati ya wachezaji bora kwa sasa katika ligi ya DR Congo hivyo kama Simba watampata basi watapata mchezaji mkubwa na mzuri sana,” kilisema chanzo hiko.