Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kuna tatizo zaidi ya kocha

Simba Vs Namungo Chama Simba kuna tatizo zaidi ya kocha

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Juzi Klabu ya Simba ilitangaza kumfungulia milango kocha mkuu, Robeto Oliveira ‘Robertinho’ baada ya kipigo ilichopata jmwishoni mwa wiki iliyopita kutoka kwa watani zao wa jadi, Yanga.

Uamuzi huo wa uongozi wa timu hiyo umekuja katika kipindi ambacho mashabiki na wapenzi wa soka hususan wale wa klabu hiyo wakijadiliana kwanini timu yao ilijikuta ikipokea kipigo kile kizito cha mabao 5-0 katika usiku uliohitimika kwa aibu kubwa Msimbazi.

Kwa mechi za watani wa jadi Afrika, matokeo kama yale huwa ni nadra sana kwa makocha kupona, japokuwa mara zote uamuzi wa kuachana nao hutoka mara nyingi katika mazingira ya kuwaonea.

Simba ni timu kubwa kwa sasa kutokana na rekodi ilizoziweka katika miaka ya karibuni barani Afrika inakotajwa kuwa miongoni mwa klabu 10 bora zenye ushawishi na pia zilizoshiriki na kupata mafanikio makubwa katika ngazi ya klabu. Hii ina maana kwamba, pamoja na mafanikio makubwa ambayo imeyapata ndani ya uwanja, lakini nje ya uwanja pia inahesabika kupiga hatua licha ya kwamba haina uwanja wala miundombinu mizuri na ya kisasa kulingana na hadi iliyo nayo sambamba na wakongwe wenzake, Yanga.

Bahati mbaya zaidi ni kwamba Simba ikiwa miongoni mwa klabu kubwa Afrika, ilipaswa kufuata nyayo za wakubwa wenzake kwa kufanya mambo yake kisasa zaidi, na hapa tunazungumzia kuhusiana na benchi la ufundi na wachezaji inaowasajili. Tusichokubaliana nacho ni kwamba Robertinho kafukuzwa kwa sababu ya kufungwa tu na Yanga. hapa wakubwa wa Msimbazi wameondoka na upepo wa mashabiki wao wakipambana kuutuliza na kuziba masikio na macho kwa kile kilichopo ndani yao.

Simba haina wachezaji wa viwangona ilipokutana na Yanga ilionekana wazi kwamba haina ubavu wa kupambana uwanjani na wapinzani wake hao. Sio kwa Yanga tu, hili limedhihirika hata wakati ikihangaika kufuzu hatua ya makundi ambapo imetinga hatua hiyo bila ushindi wowote dhidi ya Power Dynamos kwa sababu haina watu. Lakini kwa kocha, hata kama ana udhaifu wake, lakini ni huyohuyo ambaye amekuwa bora akiwafunga Yanga tangu akiwa Rayon ya Rwanda kisha Vipers ya Uganda.

Lakini kwa kuwa na kikosi chenye wachezaji waliotumika zaidi, lakini wanaokumbatiwa na uongozi bila kuongezewa wabadala wao walio mahiri, usingetemea kwa kocha yeyote kuibeba timu hiyo na kuipa mafanikio wanayotaka wakubwa. Hili ni ndoto. Sisi tunaamini katika udhaifu ambao pengine wakubwa Msimabzi wanaamini Robertinho alikuwa nao, ndimo kulikuwa na uwezo aliouonyesha akiwa na kikosi cha kawaida kuwapa matokeo katika mechi nyingi mfululizo bila kupoteza.

Bahati mbaya wakubwa wamemuona kocha huyo kuwa ndiye kikwazo cha timu yao kushinda dhidi ya Yanga, wakasahau kwamba ndani ya klabu yao kuna shida zaidi ya kocha. Na labda tunapomalizia tuwakumbushe tu kuwa, pamoja na kumfukuza kocha huyo bado hawajatibu tatizo, bali walijangalie zaidi ndani yao na ikiwezekana kiuongozi.

Chanzo: Mwanaspoti