Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kumtimua Robertinho ni kuutupa ubingwa - Mchambuzi

Robertinho Sersss Simba kumtimua Robertinho ni kuutupa ubingwa - Mchambuzi

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka kutoka EA Radio, Abissay Stephen amesema kuwa Klabu ya Simba imefanya makosa makubwa kuachana na Kocha wake, Robertinho kwani ndiye alikuwa na ramani nzima ya ubingwa msimu huu.

Abissay Stephen amesema hayo wakati akizungumzia Simba kutangaza kuachana na Robertinho baada ya kupokea kichapo cha mabao 5-1, Novemba 5, 2023 katika Dimba la Mkapa kutoka kwa watani zao Yanga.

"Mimi naweza kusema uamuzi wa kumtoa Robertinho ndio uamuzi ambao Simba wametupa kombe la ligi kuu ya NBC, kwa sababu niliongea hapa jana lile kundi la wachezaji wa Simba sio kila kocha anaweza kwenda nalo, kuna baadhi ya wachezaji uwezo wao sio tena wa kukupa ubora kwa msimu mmoja na kuendelea, yaani ndio umeishia hapo," Abissay Stephen.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live