Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kumtambulisha winga mpya mkongo baada ya Mutale

Simba Kumtambulisha Winga Mpya Mkongo Baada Ya Mutale Simba kumtambulisha winga mpya mkongo baada ya Mutale

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba inaendelea kusuka upya kikosi chake na sasa imeonyesha jeuri ya pesa katika kuwania saini ya winga wa kulia Elie Mpanzu (22), kutoka AS Vita ya DR Congo, lakini jingine ni kwamba imemtumia tiketi kwa ajili ya kuja Dar es Salaam.

Simba jana ilimtambulisha winga mwingine Joshua Mutale akitokea Power Dynamo ya Zambia ukiwa ni usajili wao wa pili baada ya Lameck Lawi kutoka Coastal Union.

Mwananchi lilikuwa la kwanza kutoa taarifa ya Simba kuwa kwenye mazungumzo na Mpanzu kutaka saini yake na huu ni mwendelezo wa dili hilo lilipofikia.

Awali Simba ilikutana na ugumu kwenye dili hilo kutokana na mabosi wa AS Vita kumng'ang'ania Mpanzu na kumuwekea dau nono, lakini Wekundu wa Msimbazi hao wakafanya umafia na tayari tiketi imeshafika mkononi kwake kwa ajili ya kumalizana Dar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live