Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kumsajili fundi Adebayor, mwenyewe yupo tayari

VICTORIEN ADEBAYOR.jpeg Victor Adebayor

Sun, 20 Feb 2022 Chanzo: ZBC2

Klabu ya Simba Sc kupitia mwenyekiti wa klabu hiyo Salim Abdallah Try Again amesema tayari wameanza kufanya mazungumzo na Wakala wa Mchezaji Victorien Adebayor raia wa Nigeria ambae Leo alikuwa mwiba mkali.

Try again anasema licha ya kwamba yupo kwa Mkopo kwasasa na timu ya Gendarmerie ila Mchezaji huyo si wakucheza Ulaya Bali ni wakucheza Simba Sc.

"Huyu ni mchezaji mzuri sana, niliongea na Rais wa USGN akaniambia yupo hapa kwa Mkopo akitokea Denmark, huyu si mchezaji wa kurudi Denmark anatakiwa kucheza Simba Sc, nitaongea na Rais tuvunje benki," amesema Salim Abdallah (Try Again).

Kwa upande wa Adebayor amesema klabu ya Simba ni kubwa Barani Afrika na ni timu nzuri. "Simba ni timu kubwa barani Afrika, kwanini usiwezekane?" Victorien Adebayor kuhusu kutua Simba Sc

Mchezo wa kundi D kombe Ia Shirikisho Afrika

Mchezo huo umemalizika kwa Simba kutoa sare ugenini na kuwa kinara wa kundi mpaka sasa.

US Gendarmerie 1-1Simba SC

G. Wilfred 13'

B. Morrison 86'

Chanzo: ZBC2