Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kumkata 'Pro' mmoja ?

Simba Tizi La Mwisho Dar Simba kumkata 'Pro' mmoja ?

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kumsajili Kiungo mkabaji, Babacar Sarr, huwenda wakalazimika kumkata mmoja ili kutimizwa takwa la kikanuni linalowataka kuwa na wachezaji 12 wa Kigeni watakaocheza Ligi ya Ndani.

Simba wanaweza pia kumuacha Sarr acheze mashindano ya Kimataifa pokee kama hawatahitaji kumkata mchezaji mmoja wa Kigeni. Au,wanaweza kumhamisha mchezaji mmoja wa Kigeni kubaki na mashindano ya Kimataifa pekee na Sarr aweze kucheza mashindano yote.

Wachezaji wa Kigeni waliokuwepo Simba kabla ya ujio wa Sarr ni Ayoub Lakred, Che Malone, Henock Inonga, Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute, Clatous Chama, Willy Onana, Luis Miquissone, Jean Baleke, Aubin Kramo na Mosses Phiri.

Dirisha dogo la usajili la Ligi Kuu ya NBC lililofunguliwa Desemba 15, 2023, linatarajiwa kufungwa Januari 15, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live