Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kumchukulia hatua Mzungu kwa kuvunja mkataba

Mzungu Dejan Simba kumchukulia hatua Mzungu kwa kuvunja mkataba

Wed, 28 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Habari wa Klabu ya Simba Ahmed Ally, amesema Klabu hiyo itachukua hatua stahiki dhidi ya Mshambuliaji wao Dejan Georgijevic ‘Mzungu’ kwa kitendo alichoamua kufanya cha kuondoka kambini Zanzibar na kutangaza kuvunja mkataba.

Nyota huyo wa Serbia alitangaza leo kupitia instagram kuwa mkataba wake na Simba umevunjika baada ya Klabu hiyo kushindwa kutekeleza yaliyo kwenye mkataba japo hakufafanua.

Lakini, Ahmed Ally amesema Dejan (28) almaarufu kama ‘Lete Mzungu’ ameonyesha kufanya jambo lisilo la kiuweledi la kutangaza kuvunja mkataba mitandaoni na kuamua kutimka kambini, hilo halikubaliki na Klabu itafanya maamuzi sahihi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live