Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kukipiga na TRA kabla ya Jwaneng Galaxy

Simba Kukipiga Na TRA Kabla Ya Jwaneng Galaxy.jpeg Simba kukipiga na TRA kabla ya Jwaneng Galaxy

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba SC wanatarajia kukipiga na TRA kwenye mchezo wa Azam Sports Federation Jumatano, Februari 28, 2024 kabla ya kukutana na Jwaneng Galaxy mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema wataanza na mechi hiyo ya Azam Sports Federation kisha kuhakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya Jwaneng mchezo uliobeba hatma yao ya hatua ya makundi.

“Kikosi kimerejea nchini na leo jioni tutaanza rasmi mazoezi kujiandaa na mchezo Jwaneng Galaxy na mchezo wa ASFC dhidi TRA ambao tutacheza Jumatano kwenye uwanja wa Azam Complex,” alisema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live