Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kukipiga na Mashujaa tena Azam Sports Federation

Simba Kukipiga Na Mashujaa Tena Azam Sports Federation.jpeg Simba kukipiga na Mashujaa tena Azam Sports Federation

Mon, 18 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mara nyingine, Simba SC atakutana na Mashuaa FC kwenye Kombe la Azam Sports Federation Aprili 9, 2024.

Hiyo ni kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania hatua ya 16 Bora ambapo Simba atakuwa ugenini huko mkoani Kigoma atakapokaribishwa na Mashujaa katika Uwanja wa Lake Tanganyika.

Ikumbukwe Simba ametoka kuwafunga 2-0 Mashujaa kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Marchi 15, 2024 katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar baada ya mchezo wa raundi ya kwanza, Mashujaa kukubali kipigo kingine cha 1-0 kutoka kwa Wekundu wa Msimbazi.

Mashujaa atakubali uteja kwa mara ya tatu mfululizo? Tusubiri muda utaongea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live