Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kukila kiporo chake na Mashujaa

Simba Kukila Kiporo Chake Na Mashujaa Simba kukila kiporo chake na Mashujaa

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wanatarajia kushuka dimbani Desemba 26, 2023 kula kiporo chake dhidi ya Mashujaa FC.

Mchezo huo wa raundi ya 6, Simba atakuwa mgeni wa Mashujaa katika uwanja wa Lake Tanganyika.

Simba akicheza mchezo huo atakuwa amelingana na Yanga kwa kucheza michezo 10 michezo lakini siku hiyo hiyo, Yanga ataanza kucheza mchezo wa raundi ya 11 dhidi ya Kagera Sugar.

Kwenye msimamo mpaka sasa kabla ya mechi hizo, Yanga ana alama 27 akiwa nafasi ya pili huku Simba akiwa na alama 22 akiwa nafasi ya tatu. Nafasi ya kwanza inashikiliwa na Azam FC ambao wana alama 28 wakiwa mbele kwa michezo, wamecheza michezo 12.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live