Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kujua mbivu au mbichi leo

Mashabiki Mkapa Simba.jpeg Simba kujua mbivu au mbichi leo

Sun, 21 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbivu na mbichi kuhusu rasimu ya mabadiliko ya Katiba ya Simba inatarajiwa kufahamika leo wakati viongozi na wanachama wa klabu hiyo watakapokutana jijini Dar es Salaama kufanya Mkutano Mkuu wa Mwaka 2023, utakaokuwa pia na ajenda nyingine ila ishu ya Katiba inatolewa macho zaidi.

Mkutano huo awali ulikuwa ufanyike Desemba, lakini kutokana na agizo la Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kutaka Simba ifanye marekebisho ya baadhi ya vipengele vya katiba, uongozi umetangaza utafanyika leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), kuanzia saa 3 asubuhi.

Licha ya mkutano huo kuwa na ajenda 11 zilizoainishwa kwenye Ibara ya 22 ya Katiba ya Simba ya mwaka 2018, ambazo ni Kuhakiki idadi ya wanachama waliohudhuria, Kuthibitisha ajenda na kumbukumbu za mkutano uliopita, yatokanayo ya mkutano uliopita, hotuba ya Mwenyekiti, kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kutoka Bodi ya Wakurugenzi.

Ajenda nyingine ni kupokea taarifa za hesabu za fedha zilizokaguliwa za mwaka uliopita, kupokea bajeti ya mwaka ya shughuli na mipango ya Simba, kufanya uchaguzi kwa nafasi zote zilizo wazi, kupokea na kujadili mapendekezo ya marekebisho ya kanuni na katiba ya Simba na kujadili mapendekezo yaliyowasilishwa na wanachama au Bodi ya Wakurugenzi.

Kwa sasa wanachama na wadau wa Simba kiu yao ni kuona rasimu ya katiba iliyopendekezwa kupitia kamati maalumu iliyopo chini ya Mwenyekiti, Hussein Kitta, ambayo tayari kulikuwa na mgawanyiko mara kamati hiyo ilipotoa taarifa majuzi na msajili kutolea ufafanuzi sambamba na wanachama wa klabu hiyo.

Kupitishwa kwa rasimu hiyo kunaelezwa kutarahisisha mchakato wa klabu kuendeshwa kwa mfumo wa hisa na kuwa kampuni ikiondokana na mfumo wa zamani wa kumilikiwa na wanachama, kwani mwekezaji atamiliki asilimia 49 na 51 zitakuwa na wanachama. Bilionea Mohammed Dewji ndiye anayetajwa kama mwekezaji wa klabu hiyo, japo mchakato haujakamilika hadi sasa ikielezwa ameweka Sh 20 bilioni kwenye akaunti.

Akizungumza nasi, Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Simba, Ahmed Ally amesema kila kitu kuhusu mkutano huo kimekamilika.

"Kila kitu kimekamilika, tunachosubiri ni mkutano kuanza tu hakuna jambo lingine kwa kuwa maandalizi yote yapo tayari."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live