Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kujiuliza kwa Dodoma Jiji leo

Simba Mazoezi 3 Kikosi cha Simba kikiwa mazoezini, kujiandaa na mchezo dhidi ya Dodoma

Fri, 1 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi kunako Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara, Simba SC, watakua katika majaribu jioni ya leo pale itakaposhuka dimbani kuwavaa Dodoma Jiji katika Uwanja wa CCM Jamhuri majira ya Saa 10:00 jioni.

Simba ambayo inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kutoa sare mchezo wake uliopita huko Musoma dhidi ya timu ya Biashara United.

Kwa upande wao timu ya Dodoma Jiji wao wanakwenda katika mchezo huo huku wakiwa na pointi tatu katika msimamo wa Ligi baada ya kuifunga Ruvu shooting siku chache zilizopita.

Dodoma Jiji rekodi zake katika msimu uliopita imekutana na Simba mara tatu, ikiwa michezo miwili ya Ligi kuu na mmoja wa Kombe la Azam Federation na katika michezo yote hiyo alipoteza.

Wakizungumza Mashabiki wa simba wameonekana kuishinikiza timu yao ihakikishe inapata ushindi kwani katika takribani mechi tatu zilizopita Simba haijafunga bao lolote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live