Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kujipima kwa Mazembe, Al Hilal

Fc05124b5c6c074be9c92bcc23785ca0 Simba kujipima kwa Mazembe, Al Hilal

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KLABU ya Simba imetambulisha mashindano mapya ya Super Cup, maalumu kwa kukiandaa kikosi chao na mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika mwezi ujao.

Mashindao hayo ya Super Cup yatashirikisha timu tatu, Simba ambao ni wenyeji, Al-Hilal ya Sudan na TP Mazembe ya DR Congo inayotarajiwa kuanza Januari 27 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alisema mchezo wa ufunguzi kikosi cha Simba kitawakabili Al Hilal Jumatano kuanzia saa 11:00 Jioni.

“Leo Simba inatangaza rasmi mashindano yanayoitwa Simba Super Cup na tumealika wageni timu ya kwanza TP Mazembe ya DR Congo, na Al Hilal ya Sudan, itaanza rasmi wiki ijayo siku ya Jumatano mechi ya kwanza Simba dhidi ya Al Hilal,”alisema Gonzalez.

Naye Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kwa mara nyingine wanaandika historia mpya kwa kuanzisha mashindano kwa kuwashirikisha mabingwa waliofanya vyema kwenye ligi za nchi zao na wanashiriki kimataifa.

Alisema matarajio yao benchi la ufundi watatumia michuano hiyo kutengeneza utimamu wa mwili ya wachezaji wao kuelekea kwenye michezo ya Ligi ya mabingwa inayotarajiwa kuanza Februari 12 ambapo Simba wataanzia ugenini dhidi ya As Vita ya DR Congo.

Alisema mashindano hayo timu zote zitatumia vikosi vyao vya kwanza na malengo yao kama timu watapambana kuhakikisha wanabakisha kombe hilo ambalo wanaamini linaandika historia.

Pia Manara alisema timu za Tp Mazembe na Al Hilal zinatarajiwa kuanza kuwasili nchini Januari 26 kuanza maandalizi kwa michezo hiyo ambayo kilele kitakuwa Januari 31 ambapo Simba watacheza na TP Mazembe.

Pia alisema leo wataanza kutaja benchi la ufundi la timu hiyo akiwemo kocha wao mkuu baada ya kuondoka kwa Sven Vanderbroeck aliyejiunga na klabu ya ASFAR Rabat ya Morocco.

Chanzo: habarileo.co.tz