Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kuitumia mechi ya Power Dynamos kujiandaa na Al Ahly

Simba Kuitumia Mechi Ya Power Dynamos Kujiandaa Na Al Ahly.jpeg Simba kuitumia mechi ya Power Dynamos kujiandaa na Al Ahly

Wed, 27 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wamesema wanaitumia mechi yao dhidi ya Power Dynamos kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya Africa Football League dhidi ya Al Ahly.

Simba anatarajia kukipiga na Power Dynamos Jumapili hii Oktoba Mosi, 2023 katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar ukiwa ni mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Afrika baada ya awali kutoka sare ya 2-2 kule nchini Zambia.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema mchezo huo wa Jumapili kwao utakuwa mazoezi kuelekea mchezo huo mkubwa dhidi ya Al Ahly.

"Tunakwenda kucheza mchezo huu tunafahamu utakuwa mgumu lakini pia kwetu sisi ni mchezo wa kujipima maana baada ya mchezo huo, mchezo unaofuata utakuwa dhidi ya Al Ahly," alisema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live